Wednesday, March 13, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe Wake Watembelea Guangzhou na Dongguan Nchini China

Mnara wa Canton wa mjini Guangzhou, China ambao una uregu wa zaidi ya mita 100.
Mtumishi katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13, 2013.  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou, China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akijaribu uzito wa spika, alipotembelea  Kituo kikubwa cha Sayansi na Teknolojia cha Ljieafun cha Guangzhou, kinachojihusisha na ubunifu na utengenezaji 'divaisi' za sauti na uchanganyaji ragi na matangazo kama ya biashara katika kumbi za muziki au vituo vya televisheni. Kulia ni Rais wa Kituo hicho,  Mike Fung na wapili kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipewa zawadi na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpa vipeperushi kuhusu utalii wa Tanzania, Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Kamishna wa Maadili wa CHama Cha Kikomunisti cha China, jijini Dongguan,  Cui Jian, katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna huyo, Machi 12, 2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Maofisa wa Mambo ya Nje wa Dongguan, China,  Sarah Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu wa NEC, CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza na Maofiwa wa Mambo ya Nje wa Dongguan Sarah Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, akizungumza na Maofiwa wa Mambo ya Nje wa Dongguan Sarah Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International  mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, wakiwa na viongozi wa Jumuia ya Watanzania waishio China, alipokutana nao Machi 12, 2013 kwenye hoteli ya Exhibition Internation mjini Dongguan, China. Kushoto ni, David Chamala (Katibu) na John Ruhembiza (Mwenyekiti) na kulia ni Abraham Merishan (Makamu Mwenyekiti) na Abubakar Mwinyi (Katibu Msaidizi).  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
 Picha Juu na Chini Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa Jumuia ya watanzania China. Picha na Bashir Nkoromo-China
--
 CHAMA Cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeeleza matumaini yake kwamba upo uwezekano wa Tanzania kupiga hatua kubwa kichumi kama inajikita kwa dhati katika kuzitumia rasilimali ilizonazo ikiwemo ardhi.

Hayo yalisemwa Machi 13, 2013 na Kamishna wa Maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), jimbo la Donguan, China,  Cuo Jian, wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, katika hoteli ya Exhibition Internation mjini hapa.


Jian ambaye pia ni Meya wa jiji la Donguan, alisema, Tanzania kama zilivyo nchi kadhaa za Afrika, inaweza kupiga hatua kiuchumi ikiwekeza juhudi zake katika kuzitumia rasilimali ilizonazo kwa kuwa rasilimali ndiyo msingi wa kwanza katika kuinua uchumi wa nchi yoyote.


Alisema, anatambuwa kwamba Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye ardhi kubwa, hivyo haina budi juhudi zake za kuinua uchumi kuzielekeza katika rasilimali hiyo ikiitumia kwa kilimo cha kisasa, kujenga viwanda na vitegauchumi mbalimbali ambavyo vitachochea kukua haraka kwa uchumi.


"Hata hivyo nawapongeza Tanzania, kwa hatua mliyofikia sasa katika kukuza uchumi, asilimia sita ya GDP, inaridhisha, la msingi serikali  kuongeza juhudi na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika juhudi hizo", alisema, Jian.


Akijibu swali na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, ambaye yupo kwenye msafara wa Kinana katika ziara hiyo, Titus Kamani aliyetaka kujua ni nini hasa China ilifanya hadi kuufanya uchumi wake ukue haraka na kuwa nchi ya pili dunia kwa maendeleo, Jian alisema, China imefikia mafanikio hayo kutokana na kuamua kuwekeza kwa nguvu zake zote kwenye rasilimali ya ardhi.


"Zipo njia nyingi za kuweza kuinua uchumi wa  nchi yoyote, juhudi hizo baadhi zinafanana na nyingine ni tofauti kutokana na nchi na nchi, lakini sisi (Wachina) tulifahamu kwamba tuna ardhi kubwa sana, hivyo tukaamua kuimua rasilimali hii kwa kila namna iliyo bora. Licha ya eneo kuwa kubwa lakini tumehakikisha hakuna eneo linaloachwa bila faida", alisema.


Kwa upande wake Kinana aliupongeza uongozi wa China chini ya chama cha CPC na wananchi wa nchi hiyo kwa kuweza kufanikisha kuinua uchumi wa nchi hiyo kwa kiwango kibwa cha sasa.


"Bila shaka ni uchapakazi usio na kikomo na wakujituma sana kwa pamoja kati ya serikali na wananchi ndiyo maana mmefanikiwa hivi, napenda kuchua fursa hii niwapongeze kwa dhati kwa mafanikio haya, nasi kama nchi rafiki tunapata kiu kubwa kuhakikisha tunafika mlipo au angalau kuwakaribia", alisema Kinana.

Kinana yupo nchini China akiambatana na ujumbe wa viongozi na maofisa wa Chama kwa ajili ya ziara ya mafunzo, katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa, na pia kudumisha urafiki wa kindugu wa siku nyingi kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo.


Katika ziara hiyo Kinana amefuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa NEC, Siasa na Uhuaisno wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Mohammed Yusuf Mohamed.


Wengine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,  Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na maofisa wa Chama. ziara hiyo


Kinana anafanya ziara  hiyo kutokana na mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China, na anafanya ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza kuifanya nje ya nchi, tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba mwaka jana mjini Dodoma.

No comments: