-
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa akisalimiana na vijana wa Boda Boda wa Arusha Mjini wakati alipokutana nao hivi karibuniNa: Happy Lazaro- ArushaWaziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani Arusha. Harambee hiyo iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la Arusha. Akizungumza katika harambee hiyo, Lowasa ambaye pia
ni Mbunge wa Monduli, aliwataka vijana kujiepusha na ushawishi wa
wanasiasa wanaowarubuni ili kushiriki katika maandamano yasiyokuwa na
tija.
Badala
yake, aliwataka wajikite katika kuzungumzia maendeleo yao. Alisema
fedha zilizopatikana katika tukio hilo, ni vyema zikatumika katika
kukopeshana ili kupanua mitaji ya biashara zao.
Comments