Rais Jakaya Kikwete Apokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi
Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa
kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano
ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es
Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia
picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya
China na Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere leo wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar
es Salaam leo.
Comments