Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akimkabidhi Tuzo kamishna mkuu wa TRA Rished Bade katika kufunga mkutano wa mwaka wa wakaguzi na wahasibu (NBAA) unaofanyika jijini Arusha ambapo TRA waliibuka kidedea katika tuzo za bodi ya uhasibu na ukaguzi kwa kuongoza kundi la taasisi za serikali kwa kutoa hesabu bora nchi nzima(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Clement Mshana akiwa anapokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima baada ya kushinda katika uandaaji bora wa mahesabu
Naibu Waziri wa Fedha Adamu Malima akiwa anamkabidhi Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allankijazi tuzo kwa kushinda katika uandaaji wa mahesabu kiwango cha kimataifa katika mfumo wa uandaaji wa viwango vinavyokubalika kimataifa
Mhasibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Layson Mwanjisi akipokea tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za mahesabu kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adamu Malima
Mkurugenzi mkuu NBAA Pius Maneno akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima
Mwenyekiti wa bodi ya NBAA Pro.Isaya Jairo akipokea zawadi kwa kufanikisha kuandaa mkutano mkubwa wa mwaka wa wakaguzi na wahasibu (NBAA)
Naibu Waziri wa Fedha Adamu Malima akimkabidhi Tuzo Mkaguzi mkuu wa ndani PPF Hosea Kashimba baada ya kushinda kwa kuwa waandaaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2013.
Comments