Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kinatarajiwa kuzinduliwa mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa kiko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahita mita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa na kiwanja hicho kiko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva na muziki wa zamani na vyakula mbalimbali vitapatikana
Comments