BARABARA DAR KUENDELEA KUIMARISHWA

Photo no 2Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Mecki Sadiki akifungua mkutano wa Wajumbe wa Baodi ya Barabara ya Mkoa wea Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa Bi.Theresia Mmbando na Naibu Waziri wa Kazi Mh.Makongoro Mahanga (kulia).(PICHA NA ARON MSIGWA -MAELEZO)
Photo na 7Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema(kushoto) na mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi wakifuatilia mkutano wa wajumbe wa Bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaamPhoto no 1Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Muhandisi J. Nyamukama akiteta jambo na baadhi ya wahandisi wa ofisi yake leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam.
photo no 4Baadhi ya wajumbe wakifuatilia masuala mbalimbali mada wakati wa mkutano huo.
Photo no 5Mbunge wa Ubungo Mh. John Myika akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es salaam.
Photo no 6Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam Mh. Idd Azzan Mh. akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es salaam.
Picha na 3. Baadhi ya wajumbe wakichangia mada wakati wa mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa miradi ya barabara katika jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawasimamia ipasavyo wakandarasi wanaojenga miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa viwango na muda uliopangwa na kuwaondolea wananchi adha ya usafiri inayotokana na ubovu wa barabara.
Aidha,amezitaka Mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaovunja sheria kwa kujenga majengo na kuta katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuziba mifereji ya maji na kubomoa kingo za mito hali inayosababisha mafuriko katika makazi ya watu wakati wa msimu wa mvua. 
Akifungua kikao cha kwanza cha wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili na kutathmini utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka 2014/2015 Bw. Sadiki amesema kuwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kutokana na ujenzi holela katika mikondo ya maji, uharibifu wa kingo za mito, na uzibaji wa mifereji unaofanywa na baadhi ya watu kwa kujenga kuta jambo linalosababisha uharibifu wa miundombinu kutokana na mafuriko wakati wa mvua. 
Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto za miundombinu ya barabara katika jiji la Dar es salaam, zaidi ya shilingi bilioni 88 zimependekezwa kuidhinishwa katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa lengo la kufanya ukarabati wa kawaida, matengenezo ya barabara za zamani na mpya kwa kiwango cha lami na ujenzi madaraja mapya na yale yaliyoharibiwa wakati wa msimu uliopita wa mvua.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua uliopita maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, ujenzi wa barabara ya Uhuru,Daraja la Kinyerezi, Ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la Machinga Complex, utekelezaji wa mradi wa barabara ya Shingofeni, Barabara ya Mombasa –Moshi bar na ujenzi wa barabara ya Ulongoni A kuelekea Kilimani.
Wamesema kuwa juhudi za usafi wa mito, madaraja na mifereji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam lazima iwe shirikishi ili mafanikio ya kuliweka jiji katika hali ya usafi na usalama wakati wa msimu wa mvua yaweze kuonekana na kuwaondolea usumbufu wananchi. 
Aidha, wamezitaka mamlaka zinazohusika katika manispaa za za Ilala, Temeke na Kinondoni kuanisha maeneo yote hatarishi katika halmashauri zao ambayo wananchi wamevamia mito kwa kujenga na kuharibu kingo za mito waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Comments