MSHINDI WA PILI WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 NDIYE ATAIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA KIMATAIFA

Miss-Universe-Tanzania
Kamati ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania 2014, Carolyne Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole chake cha mguu. Ripoti ya daktari imeonyesha kuwa kupona kwake kutachukua mwezi mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada ya siku kumi kuanzia sasa. Isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu virefu (High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na tatizo lake.

Hivyo kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili na aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala yake kama mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania 2014.
Kamati inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa nae bega kwa bega katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya mkataba wa Miss Universe Tanzania kwa mwaka mzima.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi wa Kumi na yalidhaminiwa na Insignia, Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Seif Kabelele Blog , Missie Popular blog, Urban Rose Hotel, na New York Film Academy.

Comments