Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, afanya mahojiano na gazeti la Gulf Today kuhusu kuvutia uwekezaji na kukuza utalii Tanzania
WIki iliyopita tarehe 17-18, Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii, uliandaa kongamano la uwekezaji katika sekta ya utalii, kwa nia ya kuvutia wawekezaji na watalii ili kuongeza idadi kubwa ya watalii wanao kwenda kuitembelea Tanzania.
Ubalozi Mdogo umejiwekea utaratibu katika mpango wake wa mwaka, kuandaa kongamano za uwekezaji tatu kwa kila mwaka.
Ni imani kuwa mpango huu utasaidia kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuvutia idadi kubwa ya watalii kuitembelea Tanzania na vivutio vyake.
Comments