Sehemu ya msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Sehemu ya Lori lililopata ajali
Wafanyakazi wa Lori hilo wakitafakari nini cha kufanya
Edwin Moshi wa Eddy Blog
Watumiaji wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261 BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita.
Mtandao huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama kwenye msururu huo.
Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa.
Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa.
Baadhi ya abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda mrefu(karibia siku moja).
Hali hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari.
Comments