Rais Jakaya Kikwete Akutana na Mwanamuziki Mahiri Nchini Diamond na Kumpongeza Juu Ya Ushindi Wake wa Tuzo Tano Za Muziki Za Kimataifa Mwaka Huu
Rais Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kumkaribisha na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, na kushoto ni katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.
Tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda Naseeb Abdul “Diamond” mwaka huu 2014.
Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.
Rais Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond” na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014.
Rais Kikwete akipokea CD mpya ya msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kuoneshwa tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014.
Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” juu ya ushindi wake wa tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014.
Msanii Diamond Platnumz amepata nafasi ya kipekee ya kukutana na Rais jana December 23 2014 kwenye Ikulu ya Tanzania. Diamond amekaribishwa ikulu kwenda kupokea shukrani kwa kufanikiwa kuwakilisha taifa la Tanzania vizuri kwenye tuzo tofauti nje na ndani ya africa zikiwemo za kituo kikubwa cha Tv cha Channel O zilizofanyika mwaka huu huko Afrika Kusini.
Diamond Platnumz alikuwenda na tuzo zake tano na kumuonyesha Rais Jakaya Kikwete.
Nilimuuliza manager wa Diamond ‘Bab Tale’ kitu gani Diamond alienda kufanya Ikulu?
Comments