
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Kaimu Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Maji kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka(mwenye tai nyekundu), akimsikiliza Muongozaji Ndege katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Bi. Mossy Kitang’ita, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), leo asubuhi katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka hiyo.

No comments:
Post a Comment