PINDA AKUTANA NA KIONGOZI WA KAMPUNI YA GESI YA QATAR NA KUTEMBELEA ENEO LA UJENZI WA BANDARI MPYA YA QATAR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bw. Otty Msuku ambaye ni Mtanzania , Mtalaamu wa upimaji ardhi katika mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa bandari hiyo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. Katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa Mradi huo, Don Morrison.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nPhini humo Desemba 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ya Gesi ya Qatar (Qatargas Operating Company Limited), Bw. Khalid Al Thani wakati alipotembelea ofisi kuu ya kampuni hiyo mjini Doha kujifunza uwekezaji wenye maslahi mapana ya taifa katika sekta ya gesi akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014.
Comments