WASANII WAKONGWE WAPANIA KUFANYA KUFURU KATIKA UZINDUZI WA KAONE SANAA GROUP NDANI YA DAR LIVE

Mastaa waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyopania kufanya kweli kwenye uzinduzi wa kundi lao jipya la Kaone, Boxing Day ndani ya Dar Live.
Muhogo Mchungu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni msanii Thea. 
Wasanii hao wakongwe wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo na wanahabari. Mkutano huo umefanyika jana katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Dar.
Msanii Thea (kulia) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Msanii Kingwendu akitoa burudani wakati akiongea na mwanahabari wa TBC.
ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea ule Usiku wa Wasanii Wakongwe Desemba 26 ‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, mastaa kibao waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya linalojulikana kama Kaone.
Usiku huo utakaokuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka Kaole kama vile Swebe, Davina, Koletha, Zawadi, Nyamayao, Kingwendu, Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine kibao ambao kwa mara ya kwanza watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa itakayoanza kuruka hewani Januari 4, 2015 ndani ya Runinga ya TV1.
Usiku huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha pamoja na Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo, mazingaombwe sambamba na kutoa zawadi kibao huku watoto wengine wakipata nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.

Comments