Monday, December 15, 2014

BODI YA FILAMU NCHINI YATOA WITO KWA WAMILIKI WA FILAMU KUWEZA KUWASILISHA FILAMU.

unnamedMwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) akimuonyesha stakabadhi ya malipo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo baada ya kufanya malipo ya kupata kibali kwa ajili ya filamu za kampuni hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
unnamed1
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo akiamkabidhi kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu,leo jijini Dar es Salaam.
unnamed4
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Simon Peter (kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu wanaotazama ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(katikati) na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo (kushoto) ,leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)
………………………………………………………………………….
Lorietha Laurence -Maelezo
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo ametoa wito kwa kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze kuhakikiwa na kulipiwa kwa kupata kibali cha kuingia sokoni kama sheria ya filamu ya mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.
Akizungumza katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es Salaam, Fisoo ameipongeza kampuni ya Al-Riyamy Production ambayo imeweza kutimiza wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa stamp za TRA na hivyo kuwa tayari kuingia sokoni.
Aliongeza kuwa kuna baadhi za kampuni za filamu nchini zimekiuka utaratibu na kushindwa kuwasilisha filamu zao kwa Bodi ikiwemo filamu zile zilizoigizwa miaka ya zamani ambazo zimekuwa zikionyeshwa bila kibali.
“Nimefurahishwa sana kwa namna ambavyo kampuni ya Al-Riyamy Production kwa kufuata sheria na kanuni za filamu nchini, hivyo natoa wito kwa kampuni nyingine pia kuweza kufanya hivyo ili kukuza uchumi wetu na wao waweze kufanya biashara bila usumbufu” alisema Fisoo
Naye mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala, amewaomba wasanii wenzake wenye kampuni za filamu waweze kufuata taratibu na sheria za bodi ya filamu ili kukuza soka la filamu na kuinua uchumi wa nchi yetu.
“Nawasiii wasanii wenzangu na wamiliki wa kampuni za filamu nchini waweze kufuata sheria na kanuni za filamu ili tuweze kwenda vizuri kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika ulimwengu huu wa filamu” alisema Mzee Jangala. 
Baadhi ya kampuni ambazo zimeweza kuwasilisha kazi zao katika Bodi ya filamu ,ni pamoja na kampuni ya Wananchi wote wamewasilisha filamu 119, Game First Quality filamu 35, steps Entertainment filamu 739, na Al-Riyamy Production filamu 134.

No comments: