





Le Mutuz akiwa na Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda

…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani hiyo, wadhamini na waandaaji.
Sumari alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.
“Filamu imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu, naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema Sumari.
“Filamu hiyo ina ubora wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa kipekee na kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza kuangalia, hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,” alisema.
Afisa kutoka Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Matukio mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto mbalimbali,” alisema Bodipo.
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.
Mwisho….
No comments:
Post a Comment