Balozi wa Tanzania nchini Austria ambaye ana makazi mjini Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo; mapema mwezi huu alikabidhi Hati za Utambulisho (Letter of Credence) kwa Mhe. Dkt. Heinz Fischer, Rais wa Austria. Shughuli hizi zilifanyika katika ukumbi maarufu wa Maria Teresa uliopo katika kasri ya wafalme wa zamani wa “Austro-Hungarian Empire” mjini Vienna. Gwaride rasmi kwa ajili ya Balozi mpya iliendeshwa katika viwanja vya Hofburg.
Balozi wa Tanzania nchini Austria ambaye ana makazi mjini Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo akipokea heshima kutoka Gwaride rasmi kwa ajili ya Balozi huyo ambalo katika hafla ambayo iliendeshwa katika viwanja vya Hofburg.

No comments:
Post a Comment