Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama.
Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeyahuku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba jukwaani.
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili.
Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake na wacheza shoo wake huyu amekuwa pia akifanya maonesho kama haya Ulaya na Marekani .
Mwimbaji kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa muziki wa Injili nchini Tanzania.
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakati wa tamasha hilo.
Comments