ZIARA YA KIKAZI YA WANAHABARI KATIKA UJENZI WA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI GEREZA IDETE MKOANI MOROGORO

001Mkuu wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Milioni 2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa.002Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vya Daily News, Tanzania Daima, Habari Leo na Michuzi Blogu wakifanya mahojiano na Mkuu wa Gereza Idete(hayupo pichani) walipofanya ziara yao ya kikazi Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.003Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji004Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete005Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro.006Wafungwa wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama inavyoonekana katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na trekta wakiwa gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa nchini. Kwa wastani Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Comments