MKANDARASI GEOFREY MUNGAI ATOA MSAADA WA KRISMAS KWA YATIMA DBL

Mchuungaji Mpeli  akiwashukuru wadau
Watoto yatima  wakifurahia msaada   huo
wageni  mbali mbali  waliofika katika  hafla   hiyo
Sarah Mungai na Mumewe  Geofrey wakitoa taarifa  yao fupi
 
Mmoja wa watoto yatima  akishukuru
 
Geofrey na mkewe  wakiwaongoza  yatima  kupata chakula
 
Mtoto aliyetupwa
Dr Gabone  akishiriki  chakula
Mungai akimlisha chakula  yatima 
……………………………………………………………………………………
Na matukiodaimablog
MKANDARASI Geofrey Mungai ametoamsaada wa nguo za sikukuu na chakula vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 wa kituo cha watoto yatima cha Daily Bread Life Tanzania (DBL) kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.
Mungai
alitoa msaada huo jana kwa uongozi wa kituo hicho pamoja na
kuwaandalia chakula cha pamoja watoto zaidi 39 na wananchi mbali
mbali wa mji wa Iringa kama njia ya kuwahamasisha kusaidia yatima .
Akizungumza
kwa niaba ya familia ya Mungai mke wa mkandarasi huyo Sarah Mungai alisema kuwa imekuwa ni
kawaida yake kwa kila mwaka katika msimu wa sikukuu ya Krismas na
mwaka mpya kufika katika kituo hicho na kuwapa msaada watoto hao
ili nao kuungana na watoto wenye wazazi wao kufurahia sikukuu hizo.
Hata
hivyo alisema kuwa jamii ya mkoa wa Iringa na watanzania kwa
ujumla wanapaswa kubadilika kwa kuelekeza michango yao kwa watoto
yatima ambao baada ya kupoteza wazazi wao faraja ya pekee
wanaisubiri kutoka kwa jamii inayowazunguka.
Aidha
alisema kuwa yeye kama mmoja kati ya wananchi wa Iringa wenye mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine kuweka mpango wa
kuendelea kutembelea vituo vya yatima kila mwaka kwa ajili ya
kuwasaidia misaada mbali mbali.
Alisema
kuwa upo uwezekano mkubwa wa watoto hao yatima kuendelea
kusaidia iwapo watanzania na wadau mbali mbali kuwekeza kwa watoto hao.
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho mchungaji Mpeli
Mwaisumbi mbali ya kumpongeza Mungai kwa kuendelea kusaidia watoto
hao bado wadau mbali mbali wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho .
“watoto hao wanalilewa vema na wapo ambao wanasoma shule mbali mbali na vyuo vikuu baada ya kusaidiwa na wadau”
Alisema
kuwa kituo hicho kinafanya kazi chini ya shirika lisilo la
kiserikali ya Daily Bread Life Tanzania lililosajiliwa kwa usajili
12903 chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi pia kituo
kimesajiliwa na ustawi wa jamii kwa kupewa usajili wa makao ya
watoto namba 00049995.
Hata
hivyo alisema kuwa kituo kilianza kupokea watoto 14 mwaka 2004
na sasa kuna watoto 37 waliopo kituoni hapo na kuwa toka kituo
kianzishwe jumla ya watoto 51 wamelelewa hapo
Alisema
kutokana na misaada wa wadau mbali mbali kituo kimeendelea kupata
mafanikio makubwa kama kuwa na shamba ,basi moja ,mradi wa
cherehani pia tayari shule ya sekondari
ya DBL imejengwa na imeanza kupokea wanafunzi toka mwaka huu shule iliyopo umbali wa kilomita 6 kutoka mjini Iringa kwa lengo
kuwawezesha watoto na wengine watyakaofaulu na kukosa nafasi kupata elimu ya sekondari.
Pia
alisema changamoto kubwa katika
uendeshaji wa kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi
ambako watoto hao wanasoma ,kukosa ruzuku toka serikalini na
changamoto nyingine nyingi.
Mchungaji
Mpeli aliwaomba watanzania na wadau mbali mbali pale walipo
iwapo wanahitaji kusaidia kituo hicho kutuma michango yao kupitia
 Akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007 Daily Bread Life Childreans home ,ama kwa njia ya Na M-PESA  0754362536

Comments