RAIS KIKWETE ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGURUNYEMBE MOROGORO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa
Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013
akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu
Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la
Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee
hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.…
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa
Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013
akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu
Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la
Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee
hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mjumuisho wa michango Askofu wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe
iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini
Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,
Mhashamu Telesphor Mkude katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
pamoja na kamati ya harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe
katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Magadu mjini Morogoro usiku wa
kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kwa watawa keki maalumu iliyopigwa
mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja. Aliitoa keki
hiyo kama zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa na watawa hao.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,
Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na
kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,
Mhashamu Telesphor Mkude wakiongea wakati wa harambee hiyo.
Sehemu
ya waliohudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe
iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini
Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mmoja wa wachangiaji kupiga naye picha na kuchanga shilingi milioni moja wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
(PICHA NA IKULU)
Comments