Thursday, August 13, 2015

KAMPUNI YAAFRICAN LIFE ASSURENCE YABADILISHA JINA RASMI KUWA SANLAM LIFE

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda  Akiwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius Magabe Tayari kwa Uzinduzi wa  Kampuni ya Sanlan. 
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda wa Pili Kushoto Akiwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius Magabe, wa pili kulia Pamoja na 
Mtendaji Mkuu wa umoja wa makampuni ya Sanlam.Ndugu.Ian Kirk..Israel Kamuzora, Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Mara baada Uzinduzi wa wa Kampuni ya Sanlan wakionyesha Mshikamano.
Kampuni inayoongoza katika bima za maisha nchini, African life Assurance(Aflife) jana usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.
Kwa mujibu wa Bw Magabe, Sanlam Group ni kampuni ya kuheshimiwa Afrika yenye matawi katika nchi 12. “Kwenye suala la wateja kuridhika na uaminifu, Sanlam imekuwa ikiipa sekta ya bima ya maisha kipaumbele kwa wakazi wa Afrika Kusini. Vile vile, kwa Tanzania Aflife daima imekuwa ikisifika kwa kuwa na huduma bora kwa wateja na kupewa alama za AA-na kampuni ya viwango ulimwenguni ya Global Credit Rating (GCR) kwa nguvu ya kifedha na ulipaji bora wa madai.”mabadiliko kutoka Aflife kuwa Sanlam Life Insurance yatachangia utendaji wa kibiashara kwa kampuni. “Kuna mipango ya kupanua soko la rejareja na kutoa huduma za ziada zilizo endelevu katika ukuzaji wa biashara, wateja wa Sanlam Life Insurance watapata bidhaa mpya zilizoboreshwa zaidi.”
Kupitia Sanlam, wateja wetu watakuwa na amani ya kufanya biashara na kampuni yenye masoko mengi Afrika inayoongoza katika kuimarisha ukwasi na usalama wa fedha. Tunatazamia kutumia fursa hii kuimarisha biashara yetu pamoja na uhusiano na wateja, washirika wetu, na zaidi mfumo wa Sanlam wa kufanya biashara kwa wingi na wateja. Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa Sanlam ina historia ya miaka 97 ya utendaji kazi na mahusiano bora na wateja wake. 
Bw. Kirk anaendelea kwa kusema, “Sanlam inajulikana kwa kauli mbiu ya “Wealthsmiths™” ambayo ni kielelezo tosha cha kile tunachokifanya na kuamini.Hiii na wakilisha itikadi ya uhalisia wa namna ya utendaji kazi, falsafa na uthamini wa rasilimali tunayoifanyia kazi ambayo ni fedha ya wateja wetu.Tunaelewa kiundani kuwa ukwasi unahitaji utendaji wa hali ya juu n akujitoa, kwa kutambua hili tunashirki kikamilifu na kwa umakini.” Huduma zetu zinauhalisia wa kile ambacho tunacho kithamini na pia tunafuata mfumo wa Sanlam ambao ni ujasiri, imani pamoja na ushujaa. Kwa kufuata mfumo na utamaduni huo, huduma zetu zimekuwa bora zaidi siku zote. 
Ikiwa na rekodi ya zaidimiaka 97, umoja wa makampuni ya Sanlam ina huduma tofauti za kifedha pamoja na mali zisizohamishika zenye thamani zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 60na imesambaa sehemu mbalimbali duniani. SEM(Idara Ya Masoko yanayokuwa)inawajibika kwa huduma za kifedha za Sanlam kwa biashara katika masoko yanayokuwa nje ya Afrika Kusini, na inalenga kuhakikisha utoaji endelevu wa huduma na ukuaji katika biashara mbalimbali kwa kutumia nguzo hii
Picha ya Pamoja Mara Baad ya UzinduzI huo
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda  Akitoa Hotuba yake ambapo alipongeza Kampuni hiyo kwa Kuwa Mfano wa Kuigwa na Kuitaka Kuongeza Juhudi zaidi ili kupiha hatua.
Post a Comment