Monday, January 04, 2016

WATANZANIA WATAHIMIZWA KUJITOLEA KUTUMIA HUDUMA YA NITAFUTEAPP

UNESCO
Na Nyakongo Manyama- Maelezo
Shirika la Kimataifa linalofanya kazi kupitia Tume ya Taifa Tanzania dawati la vijana U
NESCO imeanzisha huduma iitwayo NitafuteApp ili kuwezesha utafutaji, utambuzi, uokozi matibabu ya huduma ya kwanza kisaikolojia pamoja na utoaji taarifa wa watu waliopotea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji Mradi wa NitafuteApp Tryphone Elias amesema kuwa huduma hiyo ina lengo la kutafuta, kutambua na kutoa taarifa wa watu waliopotea hususani watoto, wagonjwa wenye ulemavu wa akili na wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu.
“Huduma hii itafungua uwanja mahususi wa tehama kwa familia na taasisi za kitanzania kutangaza watu waliopotea kwa ajili ya ushiriki wa jamii yote kwa ujumla katika kutafuta, kutambua, uokozi na utoaji taarifa nakuwezesha muunganiko wa jamii na familia”
Ameongeza kuwa NitafuteApp inatoa huduma kwa kuunda timu ya uokoaji, tiba za kisaikologia na huduma ya kwanza kwa wahanga wa majanga ya asili kama vile mabomu na ajali za vyombo vya majini
Pia huduma hiyo itasaidia kuboresha usalama wa kijamii wa raia kwa kuamsha hali ya umoja, usalama na maendeleo ya jamii.
Aidha ameeleza kuwa huduma hiyo itasaidia pia kuongeza thamani kwa taifa la Tanzania kwa kusambaa Afrika nzima na kimataifa kwa ujumla kwa kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili, kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kuliletea taifa fedha za kigeni pia kuleta heshima na tuzo kwa taifa kutokana na utendaji bora na kukuza matumizi sahihi ya teknologia ya mawasiliano.
Huduma ya NitafuteApp ambayo kwa sasa inapatikana katika tovuti ya www.nitafuteapp.co.tz ambayo  itafunguliwa  rasmi kiofisi na kuingia kwenye huduma za simu za mkononi 25 mwezi huu  na  na inategemewa kutengeneza ajira zaidi ya 3000 mnamo mwisho wa mwaka 2020 hivyo kuchangia kupunguza tatizo la ajira na kuchangia pato la Taifa.

No comments: