Wednesday, January 06, 2016

MAHAKAMA YA ARDHI YAWEKA ZUIO LA BOMOA BOMOA WILAYA YA KINONDONI

????????????????????????????????????
Na Raymond Mushumbusi  MAELEZO
…………………………………………………………..
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi imeweka zuio la kubomoa nyumba zilizopo katika wilaya ya Kinondoni hasa zile ambazo wamiliki wameleta ombi lao mahakamani kuzuia kubomolea.
Akitoa hukumu hiyo mbele ya walalmikaji Mwanasheria wa Serikali, mawakili wa walalmikaji na wananchi Jaji wa Mahakama hiyo kuu ya Ardhi Mhe.Panterine Kente amesema kuwa mahakama imezingatia maelezo toka pande zote mbili na kuangalia madhara watakayopata wananchi kwa kutekelezwa kwa zoezi hilo.
Jaji Panterine Kente ameongeza kuwa mahama ya Ardhi haijaweka zuio la bomoa bomoa kwa Tanzania nzima bali kwa wale tu walioleta maombi ya shauri la zuio la kubomolewa nyumba zao na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea na uwekaji wa alama za x na ubomoaji wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi na sehemu zisizostahili.
“ Nakuagiza Wakili Abubakari Salim uniletee majina yote leo hii na sio kesho ya waliofungua shauri la zuio la kutobomolewa nyumba zao ili tuweze kuendelea na zoezi la ubomoaji” Alisema Jaji Kente
Akizungumza baada ya kutolewa hukumu hiyo Wakili wa Serikali Manchare Henche  amesema wamepokea hukumu hiyo na wao wataendelea na majukumu yao ya ubomoaji wa meneo hatarishi kama Mahakama ilivyoeleza kuwa haijatoa zuio la bomo bomoa kwa Tanzania nzima ila kwa wale tu walioleta shauri la zuio.
“Tunaomba walio maeneo ya mabondeni wahame kwani zoezi hili linaendela na zoezi la uwekaji wa alama za x litaendelea kama kawaida kwa maeneo mengine nje ya haya yaliyowekewa zuio” Alisema Subuta.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutolewa hukumu hiyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia amesema kuwa uamuzi umeridhisha na pia mahakama imetenda haki kwa wananchi wa kinondoni na wanashukuru kwa kupata nafasi ya kusikilizwa kwa hoja zao.
Kesi hiyo namba 822ilifunguliwa na wawakilishi nane wanaowawakilisha  wanachi 674 ambao nyumba zao zilikuwa katika mpango wa kubomolewa  chini ya sheria za mipango miji.
Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Ardhi kutoa zuio la bomoa bomoa kwa wakzi hao kesi ya msingi itatajwa tena januari 11.
Post a Comment