Thursday, August 13, 2015

SHIWATA YAKABIDHI NYUMBA 16 MKURANGA

mku1
Wasanii wakipata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (hayupo pichani) utaratibu wa kutunza nyumba walizogaiwa kwenye kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi .
mku2
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akitoa ufafanuzi wa makazi mapya ya kijiji cha M\Wasanii Mwanzega, Mkuranga baada ya kugawa nyumba 16 kwa wasanii hao.
mku3
Wasanii wa Shiwata wakifurahia picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa nyumba katika kijiji cha wasanii, Mkuranga
……………………………………………………………………………………
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imegawa nyumba nyingine 16 kwa wanachama wake waliokamilisha ujenzi ambako mpaka sasa wanachama 120 wamekabidhiwa nyumba zao katika kijiji cha Wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.
Katika hafla ya kukabidhi nyumba hizo jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba hizo ni endelevu mpaka hapo ekari 300 zilizotengwa kwa ujenzi zitajengwa nyumba kwa mpango wa kuchangiana.
Taalib alisema aina za nyumba zinazojengwa kwa sasa ni za matofali ya saruji ya chuma kimoja kwa sh. 750,000, nyumba za vyumba viwili na sebule kwa sh. 3.8 na nyumba kubwa ya sh. mil. 6.4.
Alisema kipa wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa, Hamisi Kinye anatarajia kukabidhiwa nyumba yake Desemba mwaka huu sambamba na wasanii wengine Lilian Ndelwa, Edson Mwela, Happyness Magere, Asheri Kazeba, Jaqueline Joseph na Suzan Moshi ambao wamebadilisha nyumba walizokuwa wakabidhiwe za udongo na sasa watachukua nyumba zilizojengwa kwa saruji.
Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeandaa mpango mkakati wa kuingiza umeme na maji katika kijiji hicho kabla ya Desemba na tayari kikundi cha wasanii kimepiga kambi ya kujiandaa kurekodi tamthilia ya maisha ya Bongo katika kijiji hicho.
Mmoja wa wasanii aliyekabidhiwa nyumba ya sh. mil. 6.4, Mwajuma Kisengo alisema ametimiza ndoto yake ya kushirikiana na wasanii wenzake kuishi katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

No comments: