Monday, October 13, 2014

TAIFA STARS YAILAZA NJAA BENIN, YAITANDIKA 4-1

Watu wengi walikuwa wakiibeza sana Stars kuelekea katika mchezo wa jana dhidi ya Benin, lakini ndiyo hivyo Wahenga walisema, “mdharau mwiba, mguu huota tende” na ndicho kilichowakuta Wa Benin katika dimba la taifa licha ya kusheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama vile, Stephane Sesegnon anayekipa kunako West Bromwich Albion. 
Magoli ya Stars yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, pamoja naye Juma Luizio. Goli la kufutia kijasho la Benin Lilifungwa na mshambuliaji Sadel akipokea pasi maridadi kutoka kwake kiungo mshambuliaji, Stephane Sesegnon dakika ya 90 ya mchezo huo.
Ushindi huo ni furaha kubwa kwa watanzania ambao walikuwa wamekata tamaa na timu yao ya taifa iliyopo chini ya kocho Mholanzi Mart Nooij kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni katika michuano ya kuwania tiketi za kupangwa katika makundi ya michuano ya AFCON yatakayo fanyika mwakani nchini Moroco.

No comments:

RAIS SAMIA AFUNGUA SOKO LA KISASA KARIAKOO LILILOGHARIMU BILIONI 28, SASA BIASHARA SAA 24

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Sok...