NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI- NISHATI MHE. CHARLES KITWANGA ATEMBELEA MIRADI YA UMEME INAYOFADHILIWA NA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) KATIKA MKOA WA PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza (aliyesimama mbele) akielezea mchango wa nishati ya umeme katika ukuaji wa uchumi wa mkoa huo, katika kikao chake na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga. Mhe. Kitwanga yuko ziarani mkoani humo ambapo anatembelea miradi ya umeme inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza (kulia) akisisitiza jambo katika kikao hicho. Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, (aliyesimama) akielezea mikakati ya Serikali katika kufikisha umeme vijijini katika kikao kilichoshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza na watendaji wa Tanesco, wataalamu pamoja na waandishi wa habari.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, akisisitiza jambo katika kikao hicho
Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya (aliyesimama) akielezea mikakati ya shirika hilo katika kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme kutokana na matengenezo yanayofanyika
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha umeme cha Chalinze.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa shirika la Tanesco katika kituo cha Chalinze ya jinsi ya kuboresha hali ya umeme katika mji wa Chalinze
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na mkazi wa Kiwangwa wilayani Bagamoyo, Said Ramadhani ili kupata maoni yake kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Comments