WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI OMAN

 Moja ya barabara za jiji la Muscat, Oman
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mtenda wa Shirika la Maendeleo ya Petroli la Oman (PDO), Bw. Raoul Resticci baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya Shirika hilo ili kujifunza shughuli za uwekezaji na uvunaji wa gesi na mafuta . Alikuwa katika ziara ya kikazi nchi OmanOktoba 28, 2014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na baadhi ya mabalozi wanaowakilisha wa nchi mbalimbali  nchini   Oman katika dhifa aliyoandaliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyid Fahad Al Said (kulia) kwenye hoteli ya Al Bustan  mjini Muscut Oktoba 29, 2014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Naibu Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyi Fahad Al Said   (kushoto kwake) wakizungumza na balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh katika dhifa aliyoandaliwa Waziri Mkuu kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 28, 2014. Wapili kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus kamani na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutembelea msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na inayovutia duniani Octoba 29, 2014. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Ali Harthy zawadi ya kitabu kinachoonyesha Msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut baada ya kuutembelea msikiti huo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Oman, Oktoba 29, 2014
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  akipokea  kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy zawadi  ya kitabu baada ya kutembelea msikiti wa Sultan Qamboos Grand wa Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na yenye kuvutia duniani.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mmoja wa wafanyabiara wa Oman wanaokusudia kuwekeza Tanzania, Sheikh Abdullah Al- Zakwani baada ya kikao chake na wafanyabiashara wa Oman kwenye hoteli ya Al Bustan, Muscut Oktoba 29, 2014.
 Waziri Mkuu, MIzengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya Oman , Ahmed Bin Salim Al Harthy baada ya kutembelea  Msikiti wa Sultan Qaboos Grand uliopo Muscut ambao ni moja kati ya misiki mikubwa na yenye kuvutia sana dunianiOktoba 29, 2014. Kulia ni balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh.Yuko katika ziara ya kikazi nchini Oman

Comments