Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Professional Approach Development, Lillian
Madeje, akitoa mada kwenye kongamano hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, akihojiwa na wanahabari kuhusu ngongamano hilo. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal kwa ajili ya kufungua
kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa akihutubia katika kongamano hilo.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Hapa mdau wa mtandao huo akijisali kwenye daftari la mahudhurio.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa (katikati),
akiwa na viongozi wa mtandao huo. Kutoka kutoka kushoto, Naibu Katibu
wa mtandao huo, Daniel Stephen, Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa,
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile na Mjumbe wa Mtandao huo,
Modesta Mahiga.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
………………………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
WATANZANIA wametakiwa kujiunga katika fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza maendeleo ya nchi katika kiwango kinachostahili.
Mwito huo
umetolewa Dar es Salaam leo na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii
Mahmoud Mgimwa kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal wakati wa
Ufunguzi wa wa kongamano la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania(TPN).
Alisema kuwa ni wakati muafaka kujishughulisha na fursa za kiuchumi ili kufikia malengo ya millenia.
Alisema
Serikali inaunga mkono jithada chanya zinazofanywa na sekta binafsi
ambazo zipo kwa lengo la kuendeleza jamii na nchi kwa ujumla.
Mgimwa
aliwata Watanzania wajiunge na TPN kwani una lengo la kuwahusisha katika
sekta mbalimbali ikiwemo ujasiriamali ambao mara nyingi unakuwa katika
kukuza maendeleo ya nchi.
“Watu
wengi wanaweza kujiuliza kwamba wajiunge watapata nini lakini ukweli ni
kwamba watanufaika na taaluma ambayo itakuja kuwasaidia katika maisha
yao.
“Napenda
niwapongeze kwani nimeona vijana wengi wamejiunga na mtandao huu ambao
naamini utawasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira,”alisema.
Naye Rais wa TPN Phares Magesa alisema kuwa watu waache kusubiri kuwezeshwa badala yake wawe na mwamko wa kujiwezesha wenyewe.
Alisema lengo la sekta hiyo ni kutumia sekta ya ujasriamali katika kusaidia jitihada za Serikali kukuza maendeleo ya nchini.
“Naamini
kwamba kila kijana ambaye amehudhuria kongamano hili akitoka hapa
anaweza kuwa mtu mzuri wa kujihusisha na ujasiriamali,”alisema.
Alisema
kuwa maadhimio ya mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali
zionazpojitokeza katika jamii na kuweza kuzitatua kwa wakati.www. habari za jamii.com
Comments