Monday, October 27, 2014

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAWASILISHA MAONI MUSWADA MPYA WA VAT

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwasilisha maoni hayo mbele ya Kamati ya Bunge.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwasilisha maoni hayo mbele ya Kamati ya Bunge.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwasilisha maoni ya Shirika juu kuomba unafuu wa VAT kwa nyumba zinazouzwa kwa wananchi wa kawaida zilizo na bei chini ya shilingi milioni 100 ili Shirika liweze kuwahudumia wananchi wengi zaidi kwa kuwajengea nyumba za gharama nafuu nchini kote.
Maoni hayo yalipokelewa na Kamati ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti Andrew Chenge ambao waliyapokea maoni hayo na kuahidi kuyafanyia kazi huku wakitaka ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwamo kujua kwanini unafuu huo usiombwe kwa maeneo maalumu mathalani maeneo ya vijijini badala ya kuomba kwa kiasi cha ukomo wa fedha ambalo ndilo ombi la sasa.

Wajumbe wa Kamati hiyo walivutiwa na maoni hayo na kuomba wapewe ufafanuzi wa kina kabla ya muswada mpya wa VAT kuwasilishwa bungeni ili kuweza kuielewa dhana hiyo kwa kina kutokana na muda walioipa NHC kuwasilisha maoni kuwa mdogo.

No comments: