SWEDEN YATOA BIL. 42/- KUSAIDIA MIRADI UN

DSC_0216Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano kati ya nchi ya yake na Umoja wa Mataifa ambapo wametoa fedha kusaidia miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye ofisi za ubalozi wa Sweden jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha na Zainul Mzige MOblog).
Na Mwandishi wetu
SWEDEN imeyapatia mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini jumla ya shilingi bilioni 42/- ili kusaidia katika miradi yake ya maendeleo inayofanya nchiini Tanzania.
Makubaliano ya fedha hizo yametiwa saini jana kati ya Balozi wa Sweden Lennarth Hjelmaker na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.
Fedha hizo ambazo ni sawa na dola milioni 24, zitaelekezwa kwenye miradi ya UNDAP inayoendana na sera za Sweden za kuwezesha masuala ya utawala bora, ustawi wa jamii, wanawake na watoto na usawa wa kijinsia.
Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden, fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa Mkukuta, Mkuza na Matokeo makubwa sasa (BRN) mipango inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa .
Alisema ni matumaini yake kuwa fedha hizo zitaboresha hali ya kufanya biashara, kuwekeza kwa lengo la kutoa ajira zaidi,kuwezesha uchaguzi huru, kuimarisha huduma za jamii, kuimarisha mipango, uwajibikaji na kuimarisha mawasiliano ya radio kwa ajili ya upashanaji habari vijijini ili kusaidia maamuzi yenye mtazamo mpana zaidi miongoni mwa watu wa vijijini.
IMG_2231Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakitiliana saini makubaliano ya msaada wa fedha hizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za ubalozi huo.
Katika hafla hiyo Balozi wa Sweden alisema pamoja na kutoa fedha hizo kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, nchi yake itaendelea na makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Tanzania na kuendelea kutoa misaada yake ya kimaendeleo.
Akijibu swali la kwanini wanatoa fedha kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa pekee, na kama wameacha kutoa misaada ya moja kwa moja serikalini, Balozi huyo alisema misaada ya taifa hilo imelenga kupata matokeo yanayotakiwa na kwamba itaendelea kusaidia pia taasisi nyingine zisizo za kiserikali na serikali yenyewe.
Aidha Balozi Lennarth HjelmÄker alisema kwamba Tanzania imekuwa mfano bora kabisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwezesha ufanisi mkubwa wa miradi ya maendeleo yaliyolenga kuwawezesha watanzania kupiga hatua mbele na kuhakikisha kuwapo kwa amani.
Alisema wanafurahia kusaidia masuala ya utawala bora, kazi kwa vijana, usawa wa kijinsia na kuwapo kwa uchaguzi huru na wenye amani.
DSC_0264Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakionyesha hati za makubaliano hayo mara baada ya kutiliana saini.
Sweden imesema itaendelea kusaidia Umoja wa Mataifa nchini hasa inapotekeleza mradi wake wa misaada kwa Tanzania (UNDAP) kama mashirika hayo yalivyokubaliana na serikali ya Tanzania.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez, ameishukuru Sweden kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo.
Tanzania na Umoja wa Mataifa wanatekeleza mradi wa miaka mitano wa UNDAP ambapo mashirika ya UN yaliyopo nchini yanatoa kwa umoja wake huduma stahiki ili kupata Matokeo Makubwa.
DSC_0267Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakibadilishana hati hizo za makubaliano hayo.
DSC_0238Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden waliohudhuria hafla hiyo.
DSC_0242
DSC_0278Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za ubalozi huo jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0280Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akimtambulisha Mwandishi wa habari kutoka East Africa Radio Nassa Kingu kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya fedha hizo baina ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden nchini.
DSC_0165Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker mara baada ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden kutiliana saini makubaliano ya msaada huo.

Comments