AIRTEL YATATUA CHANGAMOTO ZA UHABA WA VITABU VYA SAYANSI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MUKULATI MKOANI ARUSHA

unnamedMakamu mkuu wa shule ya sekondari Mukulati ya mkoani arusha mwalimu Vitalisi Martine akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo.unnamed1Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mkoa wa kilimanjaro Paschal Bikomagu kushoto akimkabidhi baadhi ya vitabu vya sayansi kwa Diwani wa  kata ya Olkokola Joseph laizer  kwa niaba ya shule ya sekondari Mukulati  mkoani arusha  wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne ya shule hiyo.
……………………………………………………………….
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imeedelea kuungana na serikali katika kusaidia kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu  nchini ambapo imetoa vitabu vya ziada na kiada  katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari mukulati wilayani Arumeru mkoani Arusha
Licha ya Kada ya sayansi kuwa ndio chimbuko kubwa  la wataalamu wengi katika fani mbalimbali bado  inatajwa kutofanya vizuri kutokana na uhaba wa miundombinu na vifaa stahiki ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kada hiyo. 
Meneja wa Airtel mkoa wa Kilimanjaro  Paschal Mikomagu  akizungumzia mchango wa kampuni hiyo wakati wa mahafali ya 17 ya shule ya sekondari mukulati amesema Airtel kwa kutambua changamoto mbalimbali ndani ya kada ya sayansi nchini ikiwemo uhaba wa vitabu vya kujifunzia  imeamua kuwa na utaratibu wa kugawa vitabu hivyo.  Leo tumehudhuria mahafali  na kuchangia kutatua moja ya kero zinazokumba sekta ya elimu na tuaamini kwa msaada huu wa vitabu vitaongeza ufaulu wa wanafunzi na kusaidia shule kufanya vizuri kitaaluma
Tutaendelea kutimiza dhamira yetu kwa vitengo ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali mashuleni na kuhakikisha tunaboresha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi hadi kitabu kimoja kwa mtoto moja au wawili.
Kwa upande wake Diwani wa  kata ya Olkokola Joseph laizer  leo ni sisi Airtel imetoa msaada huu wa vitabu ambavyo vitasaidia shule hapa , lakini zaidi tunawaomba Airtel waendelee kujitolea kushirikiana nasi  na kutufadhili katika ujenzi wa maabara katika shule hii ili kuweza kufikia malengo tuliyowekewa ya kuhakikisha kila shule ya sekondari inajenga maabara kwa ajili ya mafunzo ya ziada
Akiongea mara baada ya kupokea vitabu hivyo MkeeVitalisi Martine mkuu wa shule  kwa msaada huu umeongeza uwiano wa vitabu shule hapa ambapo kwa sasa kitabu kimoja kitatatumika na wanafunzi wawili,  napenda kuwhakikishia vitabu hivi havitakaa kwenye kabati bali vitatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa ili atimaye watoto waweze kupata ujuzi kupitia vitabu hivi
Nao baadhi ya wanafunzi walito maoni yao kuhusu mchango huu shule ni hapo ambapo Happy Lyimo alisema natoa shukurani za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzangu kwa Airtel kwa kutupatia mchango wa vitabu vingi vya sayansi. Nimatumaini yangu kuwa vitabu hivi vitasaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi na  shule kwa ujumla.

Comments