Monday, October 13, 2014

KINANA AHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO IRINGA‏

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihuubia huku mkono wake ukiwa umefungwa POP, katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa, mjini Iringa jana wa kuhitimisha ziara  ya siku sita mkoani Iringa kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano na wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa, mjini Iringa kuhitimisha ziara  ya siku sita mkoani Iringa ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Wananchi wakicheza kwa furaha wakati kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
  Kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
 Ni furaha kwa kwenda mbele kadri muziki wa wimbo huo ulipokuwa unapigwa uwanjani hapo
 Nape akifarijiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo wakati wa mkutano huo
 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuelezea mipango ya chama hicho kulikomboa jimbo la Iringa linaongozwa sasa na Chadema.
 Nape akishuka jukwaani baada ya kuhutubia katika viwanja vya Mwembetogwa, Iringa Mjini
 Aliyewahi kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga wa Chadema kura za maoni, Sanga Abubakar akitangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
 Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Mdillah Sekomu akitangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM.
 Msemaji wa Bodaboda, Adam Kindole Mkoa wa Iringa,  akielezea jinsi wanavyonufaika na CCM kwa biashara yao ya kubeba abiria mjini.
Waendesha  Bodaboda wakishangilia risala iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho cha waendesha pikipiki.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia katika mkutano huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chngolo akimuaga Kinana Uwanja wa Nduli akirejea Dar es Salaam.
 Kinana akiagana na viongozi wa CCM uwanjani hapo.
 Kinana akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiingia kwenye ndege, tayari kwenda Arusha na hatimaye DSM.
 Kinana akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
 Ndege iliyombeba katibu mkuu.
Viongozi wa chama na Serikali wakipungia mkono wakati ndege iliyombeba Kinana ikipaa.

No comments:

RAIS SAMIA AFUNGUA SOKO LA KISASA KARIAKOO LILILOGHARIMU BILIONI 28, SASA BIASHARA SAA 24

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Sok...