Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiangalia Jarida katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Dunia (UNFPA – Tanzania) alipotembelea katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana leo mjini Tabora. Kutoka kushoto ni Mchambuzi wa Miradi ya Vijana na Maendeleo wa UNFPA – Tanzania Bi. Tausi Hassan na Mshauri wa Vijana wa Shirika hiloBw. John Kalimbwabo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Vijana, Jinsia, Wanawake na Watoto ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Hamisa konyesha nyaraka za vibali na sahihi za Wakuu wa Mikoa alipopita Kijana mzalendo Bw.Abiudi Denis aliyetembea nchi nzima kwa Siku 65 kwa lengo la kuhamasisha uzalendo ikiwemo kupinga Muundo wa Serikali Tatu, Kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na Kupinga watu wanaombeza Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere leo mjini Tabora wakati alipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa kijana huyo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wiki ya Vijana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitembelea mabanda wakati wa Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea katika Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Pichana Frank Shija, WHVUM
No comments:
Post a Comment