KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA WIZARA YA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS – MAZINGIRA

_DSC0041Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (aliyesimama), akizungumza na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuhusu Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi ya Bulyankulu, North Mara, Geita na Buzwagi, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa pamoja na Mbunge wa Mafia, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha(wa pili kulia).
_DSC0024Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndg. Sazi Salula (wa katikati), akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Inginia Anjelina Madete (wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini hotuba inayotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani)._DSC0039Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,wakifuatilia hotuba inayotolewa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani). _DSC0167Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika kikao cha kamati ya Bunge la Ardhi, Maliasili na Mazingira jijini Dar es saalam
wakisiliza kwa makini Taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na
Mazingira ya udhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira Dk Binilith Mahenge kwenye ukumbi wa Benki kuu leo jijini Dar es Salaam.(Picha na OMR)
_DSC0169Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dk Binilith Mahenge akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ya Udhibiti na Matumizi ya

Mifuko ya plastiki kwa Kamati hiyo. Kulia kwake ni Mh. Naibu Waziri Ummy Mwalimu akiwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Abdulkarim Esmail Shah pamoja na katibu wa Kamati Gerald Magili leo Jijini Dar es Salaam(Picha na OMR)

Comments