SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR, USIKOSE LEO THAI VILLAGE NA KESHO NDANI YA JEMBE BEACH JIJINI MWANZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA

Hashimu Donode akiimba kwa hisia kalii kabisaaa ndani ya Thai Village ili kuwapa burudani mashabiki wake.
Kama kawaida yetu kila ifikapo Ijumaa Bendi yako kali na matata hapa nchini Skylight Band tunakuwepo ndani ya kiota cha maraha Thai Village Masaki, Njoo wewe,yule na wote kuanzia mida ya saa tatu kamili mpaka mida yetu ileeeeeeeee, upate muziki mzuriiii kwenye masikio yako kwa masong makali na mapya toka kwa Timu nzima ya Skylight Band. Sogea sogea pale kati.
Digna Mbepera akiimba kwa ustadi mkubwa kabisa kutoa Burudani kwa mashabiki wake.
Kifaaa kipya machachari na moto mtoto mzuriiiiii Bela Kombo akizipiga zile vocal kaliiiii ndani ya Thai Village
Aneth Kushaba AK47 Le Meneja Her Self akichunguliaaaaaa huku akizipiga zile vocal kaliiii ndani Thai village.

Comments