MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA TANO LA KIMATAIFA KUJADILI MATUMIZI YA NISHATI ITOKANAYO NA JOTO ARDHI KATIKA NCHI ZA AFRIKA ZINAZOPITIWA NA BONDE LA UFA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo.
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili ya kabila la wamasai wakati akiondoka katika Ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo. Picha na OMR

Comments