Thursday, December 19, 2013

TAZAMA PICHA ZAIDI JINSI NDEGE YA ETHIOPIA AIRLINE ILIVYOCHIMBA UWANJA WA NDEGE ARUSHA BAADA YA KUTUA GHAFLA IKIWA NA ABIRIA 200

Muonekano wa ndege ya Ethiopian Airline baada ya kutua kwa dharura. Watu 200 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Ethiopian Airline wanusurika kufa baada ya ndege kupitiliza hadi nje ya uwanja mdogo wa ndege wa Arusha baada ya kutua kwa dharura.
Ndege aina ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la Ethiopia imetua kwa dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja cha kurushia ndege ndogo cha Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA.  Abiria zaidi ya mia mbili waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamenusurika kifo, wanasubiri msaada ngazi waweze kushushwa.
IMEHAMISHIKA KUTOKA BLOG YA PAPARAZI

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...