JK amteua Ernest Mangu IGP mpya


Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu,
Na Mwandishi Wetu,Mwananchi

Rais Jakaya Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa jana usiku na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika jeshi hilo la Polisi. Pia taarifa hiyo ilisema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).  

Comments