December 7 / 2013.
Chadema Students’ Organization (CHASO) ni umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyo chini ya Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) taifa iliyoanzishwa chini ya kanuni ya Mabaraza ya chama katika kipengele 7.8.2(a) cha katiba ya chadema
Msimamo:
Umoja wa wanafunzi wa vyuo (vikuu) wanachadema / Chadema Students Organisation(CHASO)IRINGA, unatamka rasmi wazi kwamba tunaunga mkono kwa asilimia zote maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu ya chama Makao makuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuhusiana na kuvuliwa nyadhifa za uongozi kwa baadhi ya viongozi ndani ya chama.
Tukiwa ni taasisi ya Chama inayoundwa na wanafunzi wa elimu ya juu Mkoani Iringa, tunakubaliana moja kwa moja na maamuzi ya chama, pia tunaungana na wenzetu wa CHASO Kanda ya Dar-es-salaam kulaani vikali vikundi vya kihuni vinavyotumia vibaya jina la CHASO kutoa matamko yanayopingana na maamuzi ya kamati kuu ya chama; kwani kama weledi ni wazi kwamba wanaelewa taratibu kamili zinazopasika kufikia hatima mahususi.
Maamuzi ya kamati kuu ya chama yanaonesha wazi na dhahiri kwamba Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ni chama kipevu yaani kilichokomaa na chenye misimamo yake: kisichoogopa Umaarfu wa Mtu bali ni chama kinachosimamia na kufuata misingi ya kikanuni na taratibu (katiba) iliyojiwekea.
Tunawaomba Watanzania kutoamini katika ushabiki wa kisiasa unaoendelea ama kutokuwa washabiki wa umaarufu wa mtu fulani ama kikundi fulani cha watu, katika kufikia maamuzi juu ya suala lolote katika jamii; pia tuwe wafuatiliaji na waelewa kwa kina juu ya mambo yanayohusika ili tuweze kufikia maamuzi sahihi bila upotofu (kupotoshwa).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesimamia dhana ya uwajibikaji katika ngazi zote bila kuangalia ama kuogopa nyadhifa au nafasi ya mtu, bali kuhakikisha utaratibu unafuatwa katika kufikia maamuzi bila woga, pasipo kuathiri matakwa ya kikatiba.
Watanzania wote kwa ujumla: wasomi kama dira ya jamii huu ni wakati ambao tunatakiwa kutumia uledi na busara katika kuangalia mambo(uchambuzi) kwa upeo mpevu. Ni rai kwetu kwamba si vema kutoa shutuma dhidi ya chama bila kufuatilia ama kuelewa taratibu na kanuni (katiba) zinazopasika katika kufikia maamuzi sahihi. Maamuzi sahihi sio lazima yamfurahishe kila mtu bali kulinda maslahi ya Chama na Umma kwa ujumla wake.
Watanzania hatupaswi kukurupuka kiushabiki na hurka binafsi/mihemko ama jazba na gadhabu kwani kwa kufanya hivyo tutawapa nafasi watu wenye hinda katika gurudumu la mabadiliko tunayoyaelekea hivyo tunapaswa kuwa makini.
Kimsingi tunatakiwa kuwa watu wenye Mantiki na upembuzi yakinifu katika kufikia maamuzi kwa kuzingatia uhalisia wa dhana ya uwajibikaji; hivyo basi, katika kuyaelewa mambo na tufanye tafiti za kina ili kuweza kufikia maamuzi ya kuamini watu wengine katika usahihi wake, hivyo kutozipa nafasi hisia za propaganda za mamluki.
Tunawaomba Watanzania wote katika makundi mbalimbali, kuondokana na dhana ya ushabiki katika mambo ya msingi kwani mpango wa Chadema ni kuangalia na kulinda maslahi ya Umma na siyo kujenga jina ama umaarufu wa mtu mmoja mmoja, pia chama siyo sehemu ya malumbano; hivyo shauku yetu ni kujenga wanachama Imara na siyo kupata mashabiki kabambe. Chadema itaendelea kuwa chemchemi ya Ukombozi wa Taifa na ujenzi wa viongozi wenye nidhamu, haki na uwajibikaji.
Pia tutumie fursa hii kuwaonya watu wanaotumiwa kusambaza propaganda zenye lengo la kuendeleza marumbano yasiyo na msingi.
Mwitikio wa vyama vya siasa nchini umekuwa ni watofauti kwa kuwa vinara wa kuleta mkanganyiko baina ya watanzania na uvumi wa propaganda; swali rahisi la kujiuliza wana maslahi gani juu ya maamuzi ya CHADEMA ama mtu yeyote ndani ya CHADEMA?, pia tunawataka watanzania waelewe kwamba malengo ya timu (wachezaji katika timu ni kuhakikisha wanafunga goli ili kupata ushindi mchezaji anayepiga chenga nyingi na kukimbia na mpira mpaka nje ya uwanja anakuwa hafai anapaswa kukaa benchi).
Tunawaomba watanzania tushikamane katika kipindi hiki cha mpito, tukielewa ya kwamba tunapaswa kuwa makini na propaganda zinazofanywa na makundi ya watu wenye lengo baya la kurudisha nguvu ya harakati dhidi ya mabadiliko tunayoyakusudia, kwani kila mapinduzi au mageuzi yanakwenda na usaliti. Chadema kitaenzi mawazo na mchango mzuri wa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na chama kwa maslahi ya Umma.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.
TIMOTHEO J. MKANYIA..............MWENYEKITIKITI CHASO IRINGA 0713739683
ANDEMBWISYE ISRAEL…………………….KATIBU CHASO IRINGA 0764969838
MICHAEL NOEL…………………KATIBU MWENEZI CHASO IRINGA 0716746442
MWENYEKITI CHASO
Comments