Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Emmanuel Okwi akilakiwa na shabiki maarufu wa Yanga, Steven (kulia) katika uwanja wa ndege alipowasili.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda…
Emmanuel Okwi akilakiwa na shabiki maarufu wa Yanga, Steven (kulia) katika uwanja wa ndege alipowasili.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda aliyesajiliwa na Yanga SC, Emmanuel Okwi, ametua jijini Dar es Salaam akitokea nchini Uganda.
Mamia ya mashabiki wa Yanga walihudhuria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kumpokea mwanasoka huyo mahiri aliyewahi kuichezea timu ya Simba SC.
Okwi ametua kwa ndege ya Shirika la Rwanda Air majira ya saa 10 jioni na kupokelewa na nyomi ya mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi wa timu hiyo walioondoka naye.
Okwi anatarajiwa kuungana na kikosi cha Jangwani kitakachokwaana na mahasimu wao Simba SC katika mechi ya 'Nani Mtani Jembe' Jumamosi Desemba 21 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mechi ya mwisho ya watani hao wa jadi ilimalizika kwa sare ya 3 - 3 ambapo Yanga walitangulia kufunga na Simba wakasawazisha.
Comments