Thursday, December 05, 2013

Rais Jakaya Kikwete amemteua Bwana Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar

                                                         JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huu ambao unaanzia tarehe 24 Novemba, 2013 Bwana Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Kufuatana na uteuzi huu, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Bwana Mwinchumu Hassan Salim sasa atapangiwa kazi nyingine.

Imetolewa na:
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
04 Desemba, 2013

No comments:

Prof. Mfaransa Aja na Kitabu: Aiambia Dunia Kutalii Tanzania ni Tiba

Na Mwandishi Wetu Paris, Ufaransa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, akiwa nchini Ufaransa jana Julai 8, 2025 amek...