
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni mratibu mkuu wa Tamasha la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii hadi Jumapili jijini Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza kuhusu tamasha litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mikakati yote imekamilika.
Mrisho alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James Mwang’amba, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Kwa upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young Killer, Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson Mwasabwite.
(Habari/Picha: Musa Mateja / GPL)
No comments:
Post a Comment