Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Edward Lowassa Ashiriki Tamasha Maalum la Bodaboda Jijini Dar es Salaam Apokelewa Kwa Shangwe, Vijana wa Bodaboda Wasukuma Wasukuma Gari Lake
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.
Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es Salaam,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Vijana wa Bodaboda wakilisukuma gari la Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya Furaha waliokuwa nayo.Picha Zote na Othman Michuzi
Comments