JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Aidha, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Tarime Rorya amehamishiwa Tunduru kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Comments