Thursday, December 05, 2013

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal azindua kampeni ya kupambana na malaria kupitia simu

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akizindua rasmi kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa kuhusu Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (kushoto kwake) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (wa kwanza kulia) wakishuhudia kwa karibu.Mbali na Vodacom kampeni hiyo inazihuisha pia Taasisi ya Malaria No More na Tanzania House of Talents(THT)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Walioketi kutoka kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mkurugenzi Mwanzilishi wa THTRuge Mutahaba  na Ofisa Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Georgia Mutagahywa. Kampeni hiyo inazihusisha pia Taasisi ya Malaria No More na THT.
Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Miradi ya Kijamii wa Vodafone Laura Turkington wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation.Kushoto ni Ofisa Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Georgia Mutagahywa.
Kundi la wasanii wa ngoma za kienyeji kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) wakipamba hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Mbali na Vodacom kampeni hiyo inahusisha pia Taasisi ya Malaria No More na THT.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal(wa pili kushoto walioketi) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupata bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Malaria No More Lilian Madege na Mkurugenzi Mwanzilishi wa THT Ruge Mutahaba.

No comments: