RAIS DKT. KIKWETE AENDA MAREKANI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA

 Rais Jakaya Kikwete
----
 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA  
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013

Comments