Rais Jakaya Kikwete Rais Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya Watanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru
Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.
Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.
Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya simba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.
Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
----
----
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuacha tabia ya kuwa na roho ya kulipiza visasi badala yake wawe watu wa kusamehe na kusahau kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi moja kwa moja Rais mstaafu wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela.
Rais Kikwete ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akiwa hutubia maelfu ya watu waliojitokeza kwenye sherehe za kutimiza miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe zilizofanyika katika uwanja Taifa jijini Dar es Salaam jambo ambalo si kawaida yake kutoa hotuba Rais Kikwete amesema mara baada ya Rais Mandela kutolewa gerezani hofu ilitawala Afrika ya Kusini, watu wengi wakitambua kuwa atakapochaguliwa kuwa Rais badala ya kuijenga nchi ataanza kulipiza visasi kwa wale wote waliotumika kwa namna moja ama nyingine kumtesa yeye na watu wa nchi yake.
“Badala yake Mzee Mandela alitoa tamko la kuwasamehe wote waliohusika kuwabagua watu wa Afrika ya Kusini, na kisha aliunda tume maalumu ya maridhiano ili kujenga umoja kati ya watu wenye ngozi nyeupe na wenye ngozi nyeusi, jambo hili ni la ajabu sana” amesema Kikwete.
“Hiki ni kipimo kikubwa cha ukomavu wa kisiasa, yatupasa watanzania na viongozi mbalimbali kuenzi jambo hili la kusameheana na kutokuwa walipiza visasi, hapa tulipo wengine wanasema kabisa nikichaguliwa watanikoma….. lakini nawasihi tumuenzi Mzee Mandela kwa kuiga mambo mema aliyoyafanya ambayo hadi hivi leo yamechangia kukuza uchumi wa Afrika ya Kusini, “amesema Kikwete. Amesema tokea enzi za TANU Tanzania imekuwa karibu sana na vyama vya ukombozi wa mataifa mengi Afrika, kikiwemo chama cha ANC ambacho kilikuwa kikiongozwa na Marehemu Mzee Mandela, hivyo aliwasihi watanzania waendeleze umoja huo .
“Kuna jambo moja ambalo hamlijui mwaka wa 1964 Mzee Mandela alikuja nchini na kufikia kwa mweka hazina wa TANU, Siro Swai, alikuwa akielekea kwenye mafunzo ya kijeshi Algeria, aliacha viatu vyake 'pea moja' akieleza kuwa atakaporudi atakuja kuvichukua lakini haikuwa hivyo, nilipokuwa waziri wa mambo ya nje, mke wa Swai alinifuata na kunieleza, nasi tulilazimika kuzirudisha kipindi hicho ambacho Mzee Mandela alikuwa Rais wa nchi hiyo tayari,” Anaeleza Kikwete.
Amesema haya yote yanatafsiri ukaribu na undugu wa hali ya juu kati ya nchi zetu mbili na ndiyo maana katika kumuenzi leo hii kwenye shughuli za kutimiza miaka 52 ya uhuru hatutakuwa na vikundi vya kutumbuiza. Kwa habari Zaidi ungana nasi baadaye. Ibada maalumu ya Mandela Johannesburg. Afrika Kusini, jana ilitawaliwa na ibada na maombi yaliyofanyika katika makanisa mbalimbali kuliombea taifa, baada ya kifo cha Rais wa Kwanza mzalendo, Nelson Mandela.
Comments