Friday, December 20, 2013

HIVI NDIVYO MWENYEKITI WA CCM JIJINI MWANZA ALIVYOZIKWA NA UMATI MKUBWA WA WATU..!!!

Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Padre akiongoza ibada ya mazishi katika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja akifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa Mabina.
Ndugu na jamaa wakishiriki ibada ya kumuombea Mabina.
Jeneza lenye mwili wa Mabina likiwa eneo la kaburi.
...Likiingizwa kaburini.
Ndugu na jamaa wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Clement Mabina.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo eneo la Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza.
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.

No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...