Washiriki
wa Redd’s Miss Lindi 2013 katika picha ya pamoja ndani ya ufukwe wa Lindi Beach
Resort
Redd’s
Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa leo 31 may,2013 ndani ya ukumbi wa Lindi
Beach Resort.
Jumla ya Warembo Kumi watachuana Vikali kugombania taji hilo.
wanyange hao wako kambini Hotelini hapo kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na
Redd’s Miss Lindi 2012.
Mratibu wa
Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa vizuri na warembo
wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia anataraji show itakuwa ya
Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo andaliwa, hivyo amewataka wadau
kujitokeza kwa wingi.
Viingilio
vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh
10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi
zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo
wahi tiketi yako mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo
katika mji wa Lindi.
Comments