Friday, May 17, 2013

Rais Jakaya Kikwete Azindua Kampeni Ya Lishe Jijini Dar es Salaam

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua   kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe na maendeleo yake  nchini  katika uzinduzi wa kampeni ya lishe nchini   Machi 16, 2013  katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe na maendeleo yake  nchini  katika uzinduzi wa kampeni ya lishe nchini  Machi 16, 2013  katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.Picha na IKULU

No comments: